Kwa mujibu wa ripoti ya idara ya tarjama ya Shirika la Habari la Hawza, Hawza ya Kielimu ya Jabal ‘Amil, katika ujumbe wake, imetoa rambirambi na pole za dhati kabisa kwa Imam Sahib al-Zaman (a.j.a.f.), Maraji' wakuu wa taqlidi, wanazuoni wakubwa, pamoja na wanafunzi wa Hawza za kielimu, kwa mnasaba wa kufariki Hujjatul-Islam wal-Muslimin Sheikh Ridha Mahdi.
Katika ujumbe huo imeelezwa kuwa Sheikh Mahdi aliitumia maisha yake matukufu katika kuihudumia dini na kueneza elimu ya Ahlul-Bayt (a.s), na alikuwa mfano wa mwanazuoni anayetenda kwa elimu yake, aliyepambika kwa maadili ya imani, na aliyekuwa mwenye juhudi katika nyanja za elimu na tabligh kwa ikhlasi na uwajibikaji.
Hawza ya Kielimu ya Jabal ‘Amil, sambamba na kutoa rambirambi kwa familia tukufu na wapendwa wa mwanazuoni huyu aliyefariki dunia, ilimuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu amfunike kwa rehema Zake pana, amuunganishe na Muhammad na Ahli zake watoharifu (s.a.w.w.), na aijaalie familia yake pamoja na wote waliompenda subira na utulivu wa moyo.
Maoni yako